Nay wa Mitego aoza kwenye penzi la ex wa Prezzo

Nay wa Mitego amedai amegundua mwanadada maarufu kwenye mitandao ya kijamii, Chagga Barbie aliyekuwa mpenzi wa rapper wa Kenya, Prezzo, ni mwanamke mwenye kila kigezo cha kuwa mama wa watoto wake.

Chagga-na-Nay

Nay aliyekuwa akitoka kimapenzi na msanii wa filamu Shamsa Ford na baadaye kuachana, ameiambia Bongo5 kuwa mwaka huu atafanya surprise yoyote na mpenzi wake huyo.

“Kusema kweli mimi na Chagga Barbie tunaendana sana,” amesema. “Mimi nina imani hata watoto wangu anaweza kuwalea. Suala la ndoa ni mpango wa Mungu lakini naweza kusema ndani ya mwaka huu kinaweza kutokea chochote kikubwa kwa sababu mimi natumia 966 kama codes zangu na huu mwaka ni 2016 vyote vinashabihiana. Kwahiyo naweza kusema huu mwaka utakuwa mzuri sana kwangu,” amesisitiza.

Chagga Barbie alijipatia umaarufu baada ya skendo ya kuachana na Prezzo kwa kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii.

Related Articles

Back to top button