Burudani

Nay Wa Mitego kuachia video ya ‘Shika Adabu Yako’ wiki hii licha ya BASATA kuufungia wimbo huo

Licha ya BASATA kutoa tamko la kuufungia wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ wa Nay Wa Mitego, msanii huyo ametangaza kuachia video ya huo ambao amewachana watu mbalimbali.

Nay shika adabu

Nay amesema kichupa hicho kitatoka rasmi ijumaa ya Feb 26.

“#ShikaAdabuYako 26Feb video inatoka.! Ijumaa hii.! #ShikaAdabuYako” Nay alitoa taarifa hiyo kupitia Instagram.

Wiki iliyopita BASATA ilitoa tamko rasmi la kuufungia wimbo huo (ingia hapa) kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, kashfa, uchochezi, kudhalilisha watu, na kuhatarisha amani na utengamano miongoni mwa wasanii na jamii kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents