Nchimbi aeleza jinsi anavyomkumbuka Lowassa

“Good Morning”
Hivi ndivyo alivyotusalimu Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kila alipoingia kwenye kikao chochote cha kikazi, iwe asubuhi iwe mchana au usiku alimradi ni kazi, salamu yake ilikuwa ‘Good morning’
Alimaanisha kazi inaanza wekeni kila kitu pembeni tufanye kazi.
Edward Lowassa, alikuwa kiongozi jasiri, mkweli, mpenda maendeleo na muumini wa kweli wa Muungano na umoja wa Watanzania.
Aliheshimu watu wote bila kujali rika, nafasi au uwezo wa kifedha. Akiwa rafiki yako ni rafiki yako kweli kweli.
Lowassa alikuwa kaka yangu, rafiki yangu na mwalimu wangu na mtu mwenye mchango mkubwa katika safari yangu ya Uongozi.
Namna pekee kwa Watanzania kumuenzi Lowassa ni kwa kuchapa kazi kwa bidii kwa sababu alikuwa mtu hodari kwa kutetea maslahi ya watu bila kujali wanakotoka, imani zao wala mrengo wao wa kisiasa.Tutamkumbuka kwa mchango wake katika ujenzi wa taifa letu.
Balozi Dk Emmanuel Nchimbi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).






