Bongo5 ExclusivesFahamuHabari

Ndege yawaka moto ikitua uwanjani

Siku ya Jumanne, Juni 21, ndege ya Red Air McDonnell Douglas MD-82 ilishika moto baada ya kutokea ajali ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami. MD-82.

MD-82, yenye usajili HI1064, ilikuwa ilikuwa ikitoka Santo Domingo hadi Miami International airpot ilipotoka kwenye njia ya kurukia na kuruka ndani ya eneo la nyasi kati ya barabara ya kuruka na kutua sehemu tofauti hapo ndipo ilipopoteza mwelekeo na kugonga baadhi ya vitu.

Maafisa wanasema Kulikuwa na watu 140 kwenye ndege hiyo na watatu kati yao waliripotiwa kupata majeraha madogo wakati wa kuhamishwa, wawili kati yao walipelekwa hospitali kwa matibabu Wengine waliokuwa ndani ya ndege hiyo walionekana kuwa katika hali nzuri.

Vifaa vya kwenye ndege hiyo vilifeli ilipotua kwenye uwanja wa ndege,FAA ilisema katika taarifa. Haijabainika mara moja nini kilisababisha moto huo.

Kikosi cha uokoaji cha Zimamoto kiliwahi eneo la tukio na kuweza kuuzima moto huo haraka kwa kutumia lori za povu. Ndege ilihamishwa uwanjani baada ya kuzima.

 

Miami Int’l Runway 09 na 12 zimefungwa kwa sasa.

Related Articles

Back to top button