Burudani

Ndoa iliyovunjika kwa gharama ya Tsh trilioni 1.4

Wakati watu wakiendelea kufunga ndoa za gharama, pia kuna ndoa ambazo zinaendelea kuvunjika kwa gharama kubwa. Huko nchini Uingereza aliyekuwa mke wa zamani wa mtawala wa Dubai, Princess Haya binti Hussein ametunukiwa na mahakama kuu nchini humo Pauni Milioni 554 (sawa na trilioni 1.4 Tsh) kama fidia ya talaka aliyopewa na mume wake Sheikh Mohammed Al Maktoum.

LONDON, UNITED KINGDOM – FEBRUARY 28: Princess Haya Bint al-Hussein arrives with her lawyer Baroness Fiona Shackleton at the High Court on February 28, 2020 in London, England. Princess Haya has applied for a non-molestation order and a forced marriage protection order in relation to the children she shares with with her estranged billionaire husband Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, ruler of the Emirate of Dubai. Princess Haya bint Hussein is the daughter of King Hussein of Jordan, she married Sheikh Mohammed in 2004 becoming his sixth wife. (Photo by Pete Summers/Getty Images)

Fidia hiyo ya talaka imetajwa kuweka rekodi ya kuwa ni fidia kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Uingereza, ambapo Pauni Milioni £251 itatumika kwa gharama za usalama ili kumlinda binti wa kifalme “Princess Haya na watoto wake wawili dhidi ya kutekwa nyara, na Pauni milioni 290 zitatumika kwa ajili ya matunzo ya watoto hao kwa maisha yao yote.

Chanzo cha ndoa hiyo kuvinjika kinatajwa kuwa ni baada ya Princess Haya kugundulika kuwa na uhusiano wa kimapenzi na bodyguard wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents