Habari

NEC yawarejesha wagombea wawili wa Udiwani Bwongera

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewarejesha katika orodha ya wagombea wawili wa udiwani wa Kata ya Bwongera baada ya kukubali rufaa zao zilizopinga uamuzi wa kutoteuliwa kugombea katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Juni 1, 2026.

Uamuzi huo umetolewa Mei 15, 2026 baada ya kikao maalum cha Tume kilichosikiliza sehemu ya rufaa tano zilizowasilishwa kwa mujibu wa kifungu cha 65(7) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya 343.

Wagombea waliorejeshwa ni Anastazia Peter Bampiga wa Chama cha UPDP pamoja na Ramlath Ramadhan Abdul wa Chama cha NLD, ambao walikuwa wakipinga uamuzi wa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata ya Bwongera wa kutowateua kuwa wagombea wa udiwani.

Kutokana na uamuzi huo, wagombea hao sasa wanaruhusiwa kuendelea na shughuli za kampeni kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo.

Aidha, NEC imesema bado inaendelea kushughulikia rufaa tatu zilizobaki, ambazo zinatarajiwa kusikilizwa na kutolewa maamuzi katika kikao kingine cha Tume

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents