Habari
Neema Gosple jukwaa moja na Kinondoni Revival Choir

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea ibada ya Revival Season itakayofanyika tarehe 6 Februari 2026 katika CCC Upanga, Dar es Salaam, mwanakwaya wa Kinondoni Revival Choir, Suzette Mkenzie, kwa niaba ya kwaya amesema “Neema Gospel Choir, sisi tunaweza kuwa kaka zao na dada zao, lakini Mungu amewafungulia milango mapema zaidi.
Tunaona mapinduzi makubwa waliyoyafanya kwenye tasnia ya muziki wa injili, hivyo tutakuwepo nao.Mwingine anaweza kushangaa kuona Kwaya ya Revival na Neema Gospel Choir zikiwa jukwaa moja, lakini asiogope jukwaa ni kubwa vya kutosha kuhimili kwaya zote mbili.”





