HabariMichezo

Neymar anaongoza kwa kuchezewa madhambi World Cup Qatar

Neymar ndiyo mchezaji aliyechezewa rafu nyingi zaidi mpaka sasa kwenye michuano ya Kombe la Dunia Qatar 2022.

Staa huyo wa Brazil amechezewa madhambi zaidi ya mara tisa (9) dhidi ya Serbia.

Dakika ya 79 Neymar ametolewa kwenye mchezo huo kufuatia majeraha ya ankle.

Kwa mujibu wa daktari wa timu, Rodrigo Lasmar Wabrazil watalazimika kusubiria saa 24 hadi 48 kufahamu hatma ya majeraha ya nyota huyo.

Related Articles

Back to top button