Neymar kurejea Barcelona ni sawa na Ngamia kupenya kwenye tundu la Sindano ?

Rais wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain, Lenardo ili kuhakikisha wanamrejesha tena Neymar La Liga lakini inadaiwa kuwa matajiri hao wa Ufaransa PSG wamekataa katakata kumuuza nyota huyo.

Josep Maria Bartomeu anaonekana kukata tamaa juu ya kumrudisha Neymar Barcelona baada ya kumuuza PSG. Inadaiwa mshambuliaji huyo wa taifa wa Brazil kwa upande wake anatamani kurejea Barca.

Paris St-Germain ipo katika hatari ya kuwapoteza nyota wake wawili Neymar na Kylian Mbappe kwa wakati mmoja kwenye dirisha la usajili lijalo huku mikataba yao ikiwa inakaribia kumalizika.

Neymar mwenye umri wa miaka 27 anatamani kucheza tena na Lionel Messi na Luis Suarez ili kurejesha upya MSN ndani ya Camp Nou.

Wengi wanaamini kama Neymar atarejea Barcelona ataweza kumshawishi Messi kusaini mkataba mpya ambao mpaka sasa amegoma kutia wino.

Related Articles

Back to top button