Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

Ngoma mpya ya Beyonce ‘Heated’ iliyoandikwa na Drake yakosolewa vikali

Wote tunafahamu kuwa staa wa muziki nchini Marekani Beyoncé Giselle Knowles-Carter alimaarufu kama Beyoncé ameachia album yake mpya Renaissance ambayo inafanya vizuri kwa sasa kote ulimwenguni.

Baada ya album hiyo kutoka Beyonce anakabiliwa na ukosoaji kwa kutumia maneno ya kukera katika baadhi ya nyimbo kwenye albamu yake mpya, Renaissance.

Neno la dharau, ambalo mara nyingi hutumika kurejelea watu wenye ugonjwa wa kupooza kwa ubongo, limetumika mara mbili katika wimbo wa ‘Heated’, ambao umeandikwa na nyota wa Canada Drake.

Hili linatokea wiki chache tu baada ya nyota wa pop wa Marekani Lizzo kuomba msamaha kwa kutumia neno moja katika wimbo wake GRRRLS.

Baada ya tukio hilo, wimbo wa Beyoncé ‘’ni kama haujakubalika’’ anasema mtetezi wa ulemavu Hannah Diviney.

‘’Nimechoka na kufadhaika kuwa tunazungumzia hili tena mara tu baada ya kupata jibu la maana kutoka kwa Lizzo,’’ anasema mwandishi wa BBC wa walemavu Nikki Fox.

‘’Lakini ni neno la kutisha. Ni neno ambalo hatutawahi kulitumia nchini Uingereza – ingawa tunatambua wakati mwingine linatumika tofauti nchini Marekani.’’

Fox anabainisha kuwa wimbo huo una waandishi 11, na ungeondolewa na watu kadhaa katika ngazi ya kurekodi kwenye label ya Beyoncé.

‘’Ukifikiria wimbo huo umepitia watu wangapi na hakuna hata mmoja wao aliyefikiria,’’ Subiri kidogo, na pia hakuna hata mtu mmoja ambaye hakufahamu wakati Lizzo alitumia neno moja. Inasikitisha sana.’’

Albamu ya Beyoncé inatarajiwa kushika nafasi za juu licha ya utata huo.

Related Articles

Back to top button