Ng’ombe wote nchini Uganda kupatiwa vyeti vya kuzaliwa, Sababu za kibiashara zatajwa

Katika kutimiza masharti ya kibiashara ya Soko la Muungano wa Ulaya, EU. Ng’ombe wote nchini Uganda wanatarajiwa kupewa vyeti vya kuzaliwa ili kukidhi vigezo na masharti ya soko hilo.

Hatua hiyo, imetangazwa na Waziri wa kilimo na Uvuvi, Vincent Ssempijja ambaye amesema kuwa masharti mapya ya soko hilo, yanataka kila bidhaa inayoingizwa sokoni lazima ijulikane imetoka wapi? Imezalishwa na nani? na maelezo mengine muhimu.

Wakulima watasajliliwa na bidhaa zao kupewa nambari maalum ili kurahisisha mchakato wa kibiashara kati nchi hiyo na mataifa mengine hasa yale ambayo ni wanachama wa Muungano wa Ulaya, Hatuwezi kunufaika katika masoko makubwa hadi wakulima wetu wasajiliwe na bidhaa zao sijajiliwe ,“amesema Waziri Ssempija.

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo, Imeeleza kuwa wakulima watasajiliwa kivyao na Mifugo ikiwemo ng’ombe watapewa cheti cha kuzaliwa kwasababu waagizaji bidhaa za nyama wanahitaji nyama kutoka kwa ng’ombe walio na na miezi kati ya 15 hadi 24.

Kwa mujibu wa tovuti ya gazeti pendwa la Daily Monitor, Imeelezwa kuwa bidhaa za Uganda zinazopelekwa kwenye masoko ya Ulaya huwa zinazuiliwa au kurudishwa kwa kutokukidhi masharti

Sekta ya kilimo nchini Uganda inachangia 70% ya ajira zote nchini Uganda.

Hata hivyo, Taarifa iliyotolewa na Rais Museveni, Kupitia kwa Waziri Mkuu wa Taifa hilo, Dkt. Ruhakana Rugunda amesema kuwa usajili huo hauna lengo la kukusanya kodi za wakulima na wafugaji, bali una lengo la kuboresha bidhaa ili kuendana na ushindani wa masoko ya kimataifa.

Bado haijaelezwa kama vyeti hivyo vya kuzaliwa na vile vya usajili kwa wakulima vitatozwa gharama ya Shilingi ngapi? Lakini serikali imesema itaweka kiasi cha kawaida ili wafugaji waweze kumudu usajili.

Chanzo: BBC – Cows for Uganda go start to get ‘birth certificate’

Related Articles

Back to top button