HabariMichezoSiasa

Nguvu ya michezo, Rais Biden alipiga goti Ikulu mbele ya wachezaji wa Golden State Warriors

Siku ya jana timu ya mpira wa Kikapu kutoka San Fransisco Marekani Golden State Warriors walifanikiwa kwenda Ikulu kama utamaduni wa Marekani baada ya kuwa mabingwa wa ligi ya NBA.

Wakati wapo Ikulu ya White House na walipomaliza ziara yao ulifuata muda wa picha,

Rais wa Marekani Joe Biden na makamu wake Harris walionekana wakijadili jinsi picha hiyo itachukuliwa. Rais kisha akainama kwa kupiga goti moja, na kocha wa Worriors Steve Kerr alioonekana akisema, “Hapana,” na kutikisa mkono wake wa kulia ili kumpungia asifanye hivyo lakini Rais akatabasamu, na makamu wa rais akacheka huku akiwa amepiga goti moja.

“Sifanyi hivyo,” Harris alisema na tabasamu.

Kisha Harris akaingia kati ya nyota wa Warriors Steph Curry na mkongwe Andre Iguodala huku picha zikipigwa.
Hii ndio nguvu ya michezo duaniani mara nyingine viongozi wanajiondoa wadhifa wao na kuonyesha namna michezo inavyotakiwa kusapotiwa kimichezo michezo zaidi.
Wengi wanasema michezo inaiunganisha dunia nzima.
Link ipo chini hapo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents