Habari

Ni marufuku kusafirisha mchanga nje ya nchi – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amepiga marufuku usafirishaji wa mchanga wa madini nje ya nchi na ametaka mchanga wote ufanyiwe uyeyushaji hapa hapa nchini.

Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo wakati akiweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Kampuni ya Goodwill Tanzania Ceramic Limited kilichopo katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.

“Tunauchukua mchanga tunausafirisha mpaka nchi nyingine ya mahali fulani, sasa ni marufukku kusafirisha mchanga inawezekana matangazo haya yako live Waziri Muhongo unisikilize leo, hakuna kusafirisha mchanga kwenda nje, tuulinde hapa mchanga tujenge kiwanda cha kuchuja, tutakuwa tunaona kuliko kupeleka nje ya Ulaya huko wanakuchujia wao, yaani Mungu ametubariki mno madini hayaishi, yangekuwa yashaisha, nchi hii imebarikiwa kila kitu kiwanda hiki tukitunze,” alisisitiza.

“Nchi hii tumechezewa vya kutosha, sasa nyinyi hapa mnayeyusha mchanga kwa kuuchemsha hadi nyuzi joto 1,000 wakati wengine wanasafirisha mchanga nje ya nchi wakati uchemshaji wake hauhitaji kufika hata nyuzi joto 1,000, naiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Nishati na Madini kuwa kuanzia sasa ni marufuku kusafirisha mchanga nje ya nchi.”

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents