Ni Simba Vs TP Mazembe kwa Mkapa Simba Day 2021

Mabingwa wa Nchi, Simba SC imetangaza kucheza na miamba ya soka barani Afrika klabu ya TP Mazembe kutoka DR Congo kwenye siku ya Simba Day iliyopangwa kufanyika Septemba 19, 2021.

Simba itawakabili Mazembe kwenye mechi hiyo ya kirafiki ambayo pia itatumika kutangaza wachezaji wao wapya waliyosajiliwa msimu huu pamoja na burudani mbalimbali.

Itakuwa mara ya pili kwa Mnyama kukutana na TP Mazembe kwa mwaka huu, kwani wawili hao waliwahi kucheza Simba Super Cup na kutoka sare ya bila kufungana.

 

Related Articles

Back to top button