Burudani

Nicole afikishwa Mahakamani shuhudia

Mwigizaji Joyce Mbaga, anayejulikana pia kama Nicole Berry, amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kivukoni/Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na kuendesha biashara haramu ya upatu. Inadaiwa kwamba Nicole aliwahamasisha watu kujiunga na makundi ya WhatsApp kwa ahadi ya kupata faida kubwa kwa muda mfupi baada ya kuchangia fedha. Hata hivyo, baada ya kupokea michango hiyo, alikosa kupatikana kwenye simu na kuwafanya wanachama kukosa fedha zao.

Nicole anashitakiwa na mashtaka matatu

1. Kuendesha biashara ya kijinai kwa lengo la kujipatia pesa bila kuwa na leseni halali kutoka Benki Kuu. Hii inamaanisha alikuwa anafanya shughuli za kifedha bila ruhusa rasmi.

2. Kupokea amana zenye thamani ya milioni 100 bila kuwa na kibali au leseni inayohitajika. Hii ni kinyume na sheria za kifedha na udhibiti wa taasisi za fedha.
Kuendesha mfumo wa malipo bila kuwa na leseni halali ya malipo iliyotolewa na Benki Kuu. Hii inahusisha kufanya miamala au kuanzisha huduma za malipo bila kibali kinachotakiwa.

Video Nzima ipo katika Akaunti yetu ya youtube ya Bongo5

Written edited by #abbrah255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents