Habari

Nidhamu yaondoa polisi 156

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema takribani askari Polisi wanafunzi 156 wamefukuzwa mafunzo ya kijeshi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za utovu wa nidhamu na kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya shule ya Polisi.

”Toka mmekuja kuanza mafunzo, takwimu nilizonazo takribani askari 156 wanafunzi wamefukuzwa jeshi, wamefukuzwa jeshi kwasababu ya utovu wa nidhamu, wamefukuzwa jeshi kwasababu ya kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya chuo cha jeshi la polisi.”- amesema IGP Sirro

IGP Sirro amesema hayo wakati alipofanya ziara kwenye uwanja wa medani za kivita wilaya ya Siha, West Kilimanjaro katika Shule ya Polisi Tanzania, ambapo pia amewaelekeza wanafunzi hao wa kozi ya awali ya askari Polisi kufuata sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ikiwa pamoja na kudumisha nidhamu ndani ya Jeshi la Polisi.

Source: Channelten

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents