Nigeria yawapiga ‘Stop’ wasafiri kutoka India, Brazil na Uturuki

Kamati ya rais ya kupambana na janga la Covid-19 nchini Nigeria, imesema taifa hilo litapiga marufuku wasafiri wanaokuja kutoka India, Brazil na Uturuki, kutokana na kuenea pakubwa kwa virusi vya corona katika mataifa hayo.

Taarifa ya mwenyekiti wa kamati hiyo Boss Mustapha, imesema watu walio na hati za kusafiria zisizo za Nigeria na wasiokuwa wakaazi wa taifa hilo waliozuru mataifa yaliotajwa katika kipindi cha siku 14 kabla ya kwenda Nigeria, watanyika ruhusa ya kuingia nchini humo, kuanzia Mei 4.

Nigeria imetangaza visa vipya 43 vya maambukizi ya virusi vya corona jana Jumamosi, na kufanya jumla ya visa vyake kuwa 165,153, na vifo 2,063.

Related Articles

Back to top button