Michezo
Nilikuwa sikupendi hata kidogo – Viera
“Kwa miaka tisa niliyocheza Arsenal nilikuwa sikupendi hata kidogo. Ni kweli, nilikuwa siwezi kukuvumilia kwa sababu ulikuwa ukimpiga mateke kila mtu hasa Robert (Pires) alipokuwa pale…
Na katika mechi ile nikasema, ni lazima nihakikishe unatambua kwamba leo, hautamgusa Robert kwa sababu nilijua ule ulikuwa ndio mpango wako kwa sababu Robert alikuwa anakusumbua sana,” kauli ya nahodha wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira, akisimulia tukio maarufu la mwaka 2004, alipogombana na Gary Neville lililofanya Roy Keane kuingilia kumtetea nyota mwenzake wa Man United na nusu Vieira na Keane wazichape.