Burudani

Nililazimishwa kuolewa nikiwa mdogo sana – Christina Shusho

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Christina Shusho (46) amesema kuwa aliolewa na mchungaji John Shusho akiwa na umri mdogo wa miaka 19 tu na alikuwa mrembo.

Mkali huyo wa nyimbo za Hapo Mwanzo, Ushirika na Wewe, Wa Kuabudiwa, Mtetezi wangu, Shusha Nyavu, Relax, Teta Nao, Bwana Umenichunguza na nyingine nyingi anasema;

“Niliolewa na mtu mmoja lakini nilikuwa nahudumia ndugu wa mume wengine nane, nilikuwa mrembo lakini nilikuwa mjinga kichwani. Nikajiuliza hivi nimeolewa au ni mfanyakazi wa hawa watu? Sasa hivi sina ule uzuri tena lakini kichwani Niko Smart, najielewa na Kujitambua.

“Nimeolewa nikiwa na miaka 19 nilipomaliza kidato cha nne nilikuwa mrembo sana, msinione hivi ni vile nimechoka tu, nilikuwa nikipita hivi wanaume walikuwa macho yote kwangu. Uzuri wangu ulimpa hofu mama yangu alikuwa anawaza huyu mtoto  na uzuri huy akikiaa hapa si ataharibika.

“Basi akajitokeza mzee Shusho akasema nataka kuoa huyu binti, mama hakutaka maelezo akasema chukuaaa chukuaaa chukuaaaa chukuaaa chukuaaa!!!!! Asituharibikie hapa, kwa hiyo niliolewa nikiwa na miaka 19 pekee.

“Nilikuwa mdogo na sikuelewa nini maana ya mapenzi wala sikujua maana ya Upendo, naweza sema nililazimishwa kuolewa ili nisiharibike lakini si kwa matakwa yangu” alisema Christina Shusho.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

cc: TanzaniaWeb.Live

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents