Siasa

Nitakwenda MSD na Polisi, TAKUKURU – Majalaiwa amtaka Mkurugenzi amkute ofisini

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amkute katika ofisi za Bohari ya Dawa (MSD) Jumatatu saa nne asubuhi, baada ya kubaini madudu katika ununuzi wa vifaa vya matibabu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo katika ufunguzi wa Wiki ya Ununuzi wa Umma jijini Arusha ambapo ametaja gharama kubwa iliyotumika kununua vifaa hivyo tofauti na bei halisi za soko, na hivyo kupoteza fedha nyingi za umma na kuwakosesha wananchi huduma kwani vifaa vilivyonunuliwa ni vichache.

Akizungumza na wataalamu wa ununuzi na ugavi, ametaja baadhi ya manunuzi hayo kama vile ununuzi wa seti moja ya vitenganishi kwa ajili ya awamu moja ya kusafisha damu kwa shilingi 65,000, lakini wakanunua kwa shilingi 189,000.

Aidha, MSD walitakiwa kununua mashine ndogo ya kipimo cha haemolojia ya mwili kwa shilingu milioni 5, lakini wakanunua kwa shilingi milioni 14,045,000.

Ametoa mfano mwingine ambao ni kipimo kikubwa cha haiemolojia ya mwili ambacho ni shilingi milioni 37, lakini MSD wamenunua kwa shilingi milioni 147.9, pia walitakiwa kununua mashine ya kuchakata maji kwa ajili ya kusafisha damu ambacho kinauzwa milioni 32 lakini wamekinunua kwa shilingi milioni 129.

“Kwanini hili linatokea? kwa maslahi ya nani?” amehoji Waziri Mkuu

Kutokana na PSPTB kuwa na jukumu la kuwachukulia hatua wataalamu wa ununuzi na ugavi wanaokiuka sheria, Waziri Mkuu Majaliwa ameiagiza kufika ofisi za MSD akisisiitiza kuwa serikali haiwezi kukubali hali hiyo kuendelea.

“Na mimi sitasita kwenda na Kamanda Sirro, na Kamanda Hamduni, ili washughulike na watu. Lazima tuanze na watu hawa wanaofanya kazi hii, wakae nje, hatua nyingine zifuate,” amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa

Ameongeza kuwa pengine wasimamizi wa vitengo vya ununuzi na ugavi wanahitaji kuapishwa, kutokana na unyeti wa nafasi zao katika kutoa huduma kwa Watanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents