HabariMichezo

Nitamleta Messi Aston Villa, nipo tayari kukatwa mshahara

Mlindalango wa Klabu ya Aston Villa, Emi Martinez amejitolea kukatwa sehemu ya mshahara wake ili kuisaidia timu hiyo kumsajili, Lionel Messi.

Emi Martinez ambaye pia ni goli kipa wa timu ya taifa ya Argentina ameyasema hayo wakati wa mahojiano yake na ESPN.

“Kama [mashabiki wa PSG] watampigia mayowe Messi, nitamleta Villa. Njoo hapa, tutakulisha, mimi hula nyama choma kila wikendi.”- Maneno ya Martinez akizungumza kwa utani.

”Nitakata mshahara wangu, tutafanya kila liwezekanalo.”

Messi mwenye umri wa miaka 35, amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka Paris Saint-German kumfuata mshindai wake Cristiano Ronaldo kunako Ligi ya Saudia.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents