Habari

Njombe yajivunia kupata Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Njombe yajivunia kupata Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kinachojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambayo itakuwa Taasisi ya Kwanza ya Elimu ya Juu katika mkoa huo.

 

Akizungumza Septemba 20, 2024 mkoani Njombe wakati wa kuanza kwa ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita, Mbunge wa Jimbo hilo Deo Mwanyika amesema kuwa uamuzi wa ujenzi wa kampasi hiyo utakuwa mkombozi kwa wananjombe katika kupata elimu ya Juu.

 

Aidha, ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu wananjombe wameshuhudia uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu ambapo shule mpya za msingi saba, sekondari 12 na mabweni 107 yamejengwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents