Habari

NMB bonge la mpango yaanza kwa kishindo, 10 wazoa fedha na pikipiki mbili

Droo ya kwanza ya Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde inayoendeshwa na Benki ya NMB iitwayo Bonge
la Mpango, imefanyika ambako washindi 10 wameshinda pesa taslimu na wawili wakijitwalia pikipiki ya
tairi tatu aina ya Lifan Cargo.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya weka ushinde Bonge la Mpango inayoendeshwa na Benki ya NMB. Kushoto ni mwakilishiki kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga na kulia ni Afisa Huduma kwa wateja wa benki ya NMB, Neema Deusi.

NMB Bonge la Mpango, inalenga kutambua na kuthamini utamaduni chanya wa wateja kujiwekea akiba,
ikiwa ni pamoja na kurejesha sehemu ya faida ya benki hiyo kwa mwaka uliopita, ambako NMB ilipata
faida ya zaidi ya sh. Bilioni 205.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Ally Ngingite, aliwataka
wateja wa benki hiyo kuendelea kujiwekea akiba mara kwa mara, ili kujishindia zawadi mbalimbali zenye
thamani ya sh. Milioni 550.

Ngingite alibanisha kuwa, ukiondoa pesa taslimu wanazoshinda wateja wa kila wiki, NMB Bonge la
Mpango pia inawawezesha wateja wawili wa kila wiki kushinda pikipiki ya mizigo, gari dogo la mizigo
aina ya Tata 'Kirikuu' na Toyota Fortuner.

"Ukiweka kuanzia Sh. 100,000 anakuwa na nafasi ya kushinda pesa taslimu, pikipiki ama kirikuu na wale
ambao akaunti zao zitakuwa na akiba isiyopungua Sh. Milioni 10, watashindania Toyota Fortuner ya Sh.
Mil. 169," alisema Ngingite.

Kwa upande wake, Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga,
aliipongeza NMB kwa kampeni zilizobeba uwezeshaji kwa wateja, huku akiwahakikishia washiriki kuwa
droo hizo zinafuata taratibu zote. Lakini pia aliwahakikishia wateja kuwa hakuna ubabaishaji wowote.


washindi watapatikana kutokana na bahati zao tu na si vinginevyo, hivyo wawe huru kushiriki na
watashinda," alisema Semasenga. Washindi wa LIFAN Cargo ni Martha Mathew Mmasi wa Dar es Salaam na Willy Moses Mwasaka wa
Tukuyu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents