Habari

NMB teleza kidijitali ndani ya A-town

Kwa mara nyingine tena, Benki ya NMB katika kuendeleza ubunifu na kuwarahisishia huduma wateja wake,
inaendelea kuinadi kampeni ya Teleza Kidijitali iliyozinduliwa May 09, 2022 na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo,
Ruth Zaipuna, katika soko la Tandika jijini Dar es Salaam kwa kuingia mtaani na kuwaelimisha Watanzania
umuhimu wa huduma zilizo chini ya kampeni hio, ambazo ni NMB Pesa Wakala, Lipa Mkononi na Mshiko Fasta.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, NMB ilifikisha kampeni hiyo jijini Arusha, ambapo lengo kuu ni kusogeza huduma kwa
wananchi ili waweze kutumia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo nafuu.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi akizindua kampeni ya Teleza kidijitali, iliyofanyika kwenye Soko la Kilombero jijini Arusha.

Akizundua kampeni hio katika Soko la Kilombero jijini Arusha, Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa NMB,
Filbert Mponzi, alisema kampeni hio imelenga kutoa elimu ya kutosha na kuwaingiza Watanzania wengi zaidi
kwenye Sekta rasmi ya kibenki ili waweze kunufaika na huduma mbalimbali ambazo wanazitoa.

Lakini pia, aliwasisitizia kuchangamkia fursa ya Mshiko Fasta ambapo mteja anaweza kupata mikopo nafuu isiyo na
dhamana kupitia simu yake tu ukiwa na NMB Mkononi.

Aidha, Mponzi aliongezea kuwa wale wenye sehemu zao za biashara, Benki ya NMB inatoa huduma ya Lipa
Mkononi, ambayo inamuwezesha mfanyabiashara au mjasiriamali kulipwa pesa za mauzo moja kwa moja katika
akaunti yake kiurahisi na kwa usalama bila kulazimika kuhamisha fedha nyingi kutoka eneo lake la biashara kwenda
tawini.

Baadhi ya wakazi wa Arusha waliohudhuria kwenye kampeni ya Teleza Kidijitali iliyozinduliwa kwenye Soko la Kilombero jijini Arusha

“Pia, NMB Pesa Wakala, ni huduma inayomuwezesha mtu yeyote kuwa wakala kwa kupitia simu yako ya mkononi
(smart phone au tochi) kutoa huduma za kuweka, kutoa au kutuma pesa kiurahisi,” alisema Mponzi.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Kilombero wameishukuru NMB kwa kuwaletea huduma hiyo
itakayowasaidia kupata mikopo ya fedha kwa ajili ya kujiinua kichumi.

Wateja wakifungua akaunti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Teleza kidijitali, iliyofanyika Soko la Kilombero jijini Arusha.

“NMB wametuletea njia rahisi ya kufanya biashara, kwa sababu wapo baadhi ya wateja wanataka kununua kwa
njia ya kibenki, hii itaturahisishia hata hatutakuwa na haja ya kutafuta chenji. Vilevile fedha zetu za mauzo
zitakuwa salama hatutakuwa na haja ya kusafirisha fedha nyingi kuzipeleka benki,” alisema Hassan Athumani.

 

Related Articles

Back to top button