Habari

NMB yageukia wakulima, yamwaga mabilioni kwa riba nafuu

JUMLA ya Sh78.8 bilioni zimeshatolewa na benki ya NMB kwa wakulima kati ya Sh100 bilioni walizotengewa kwa
ajili ya kukopeshwa kwa riba nafuu ili kusaidia kukuza mnyororo wa kilimo.


Fedha hizo ni sehemu ya mkakati wa benki ya NMB kwa ajili sekta ya kilimo inayoajiri watanzania wengi zaidi
ambapo benki inatoa fedha hizo kwa riba isiyozidi asilimia 10.

Takwimu hizo zilitolewa jana na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Filbert Mpozi wakati akimkaribisha Rais
Samia Suluhu Hassan alipotembelea banda la benki hiyo kubwa nchini.

Kwa upande wake Rais alipongeza juhudi zote zinazofanyika ndani ya benki hiyo akisema kuwa anawashukuru sana
kwa juhudi zao hizo.

Rais alifika katika banda hilo kwenye hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani nchi nzima ambayo
ilifanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Mponzi alisema Kati ya shilingi bilioni 100 zilizotengwa kukopeshwa kwa wakulipa kwa riba ya chini ya asilimia 10,
zaidi ya shilingi bilioni 78.8 zimeshakopeshwa kwa wanufaika 3,773 huku wakiwafikia zaidi ya wakulima na
wajasiliamali wa kilimo milioni 1.4 kupitia taasisi yao ya NMB Foundation.

“Mbali na kiwango hicho, pia benki ya NMB imefanikiwa kuandaa mpango wa kufungulisha akaunti kwa wakulima,
wavuvi na wafugaji ambapo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita zaidi ya akaunti 500,000 zilifunguliwa,” alisema
Mponzi. Afisa huyo alisema lengo la njia hiyo ni kuwawekea wakulima utaratibu maalumu ili wakidhi vigezo vya
kupatiwa huduma za kifedha ikiwemo mikopo na mafunzo.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, mpango huo ni kuunga juhudi za serikali, katika kusukuma mbele agenda ya maendeleo
ya kiuchumi ya Vijana na Wanawake, hivyo waliamua kutangaza hati fungani maalumu tuliyoiita waliyoiita JASIRI
BOND.

Hati hiyo imejikita katika kuwasaidia kusaidia wanawake wajasiliamali kwa riba nafuu ambapo mwitikio umekuwa
mkubwa sana hata wameamua kuzindua NMB PESA lengo likiwa ni kurahisisha huduma za kipesa kwa wakulima na
wateja wote kuwa karibu zaidi kwenye maeneo yao.

Akizungumzia utoaji wa mbegu za mafuta alisema tayari wateja 332 wakiwemo wakulima katika vyama vya
ushirika (AMCOS) wameshanufaika na zaidi  Sh 6 bilioni  zimetolewa kwenye eneo hilo kama mikopo.
Nyingine ni kuwa benki hiyo imeshatoa zaidi ya Sh110 milioni kama mikopo ya bima ya afya za afya kwa makundi
na taasisi za wakulima 697.

Baada ya juhudi za Serikali kutangazwa katika kuongeza uzalishaji wa Mafuta nchini na kupunguza kiasi cha fedha
kinachotumika kuagiza Mafuta nje, NMB wameshafanya mawasiliano na wizara ya kilimo ili kuunga mkono juhudi
hizo na tayari wametengeneza muundo wa mikopo kwa wakulima na mnyororo thamani unaeleza jinsi ya
kuwasaidia wakulima.

Kwenye sekta ya mikopo NMB kwa kipindi cha miaka mitano wameshakopesha zaidi ya Sh1.3 trilioni kwenye
kilimo, uvuvi na ufugaji na minyoyoyo yote ya thamani. Kingine ni kuwa, wameshaandaa mpango wa kufungulisha
akaunti kwa wakulima, wavuvi na wafugaji ambapo kwa miaka miwili iliyopita, zaidi ya akaunti 500,000
zilifunguliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents