FahamuHabari

NMB yazindua kifurushi maalumu kwa ajili ya Walimu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ametoa Rai kwa benki ya NMB
kuhakikisha inawafikia watumishi wengi zaidi wakiwemo walimu ili kuwasaidia kujiendeleza kimaisha.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizungumza na walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wa kanda ya Kati Jijini
Dodoma katika siku ya Mwalimu iliyoandaliwa na benki ya NMB ikienda sambasamba na uzinduzi wa Mpango wao Maalum wa Mwalimu Spesho Mpango huo ni kwa ajili ya walimu kupata mikopo na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo nchini huku walimu wakipongeza huduma hizo.

Waziri alisema mpango huo mzuri usiishie kwa walimu 5,000 badala yake angetamani uwafikie walimu wengi na
watumishi ili kuwajengea uwezo hasa walimu ambao ndiyo chanzo cha kuwaandaa viongozi, wataalamu wa
baadae.

Alitaka NMB kusimama na walimu wakati wote ili kuwajengea uwezo akieleza kuwa jumla ya walimu 6800 wamepandishwa madaraja hivyo ni fursa kwao kuingia kwenye mikopo kwa benki ambayo inajulikana na
uendeshaji wake mzuri kuliko kukopa kwenye taasisi ambazo zinawaumiza.

Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi (watatu kushoto) akimpa maelezo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kuzindua Mpango maalum  ‘Mwalimu Spesho’ uliyozinduliwa jana Jijini Dodoma. Wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya wateja Binafsi, Aikansia Muro na Meneja kanda ya Kati Nsolo Mlozi.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi alisema walikusanya walimu viongozi 350 kwa ajili ya
kubadilishana mawazo kuboresha zaidi huduma za kibenki na kujadiliana kuhusu fursa zilizopo kwa ajili ya kundi la Walimu nchini.

“Tunaamini, walimu hawa zaidi ya 350, watasaidia kupeleka elimu watakayoipata hapa kwa wenzao na hata familia zao na jamii kwa ujumla juu ya huduma nzuri zinazotolewa na benki ya NMB, lengo ni kumfanya mwalimu kuwa na maisha mazuri wakati wote,” alisema Mponzi.

Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi (watatu kushoto) akimpa maelezo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kuzindua Mpango maalum  ‘Mwalimu Spesho’ uliyozinduliwa jana Jijini Dodoma. Wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya wateja Binafsi, Aikansia Muro na Meneja kanda ya Kati Nsolo Mlozi.

Hoja ya NMB ilianzia kwa mbunge wa Viti Maalumu, Dkt. Teya Ntala ambaye aliomba mabenki mengine kuiga
mfano wa benki hiyo kwani imekuwa ni sehemu ya kuigwa mfano kwa wanyonge.


Aidha, Benki ya NMB inatoa mikopo mingi ikiwemo bima ya kujikinga na majanga mbalimbali, mikopo ya elimu kwa walimu na wategemezi wake, mikopo ya kilimo,uvuvi na ufugaji, mikopo ya vyombo vya moto vya binafsi na
biashara na mikopo ya wakulima wadogo wadogo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents