
Timu ya Ureno usiku wa kuamkia leo imeweka rekodi ya kupata ushindi mkubwa zaidi wa magoli 9-0 dhidi ya Luxembourg kuwania kufuzu Michuano ya Euro 2024.
Cristiano Ronaldo alikosekana kwenye ushindi huo wa Kihistoria kufuatia kutumikia adhabu ya mchezo mmoja kutokana na kadi ya njano aliyopata Ijumaa dhidi ya Slovakia.
Gonçalo Ramos alichukua nafasi ya Ronaldo kwenye safu ya ushambuliaji na kufanikiwa kufunga magoli mawili kwenye ushindhi huo mnono.
Mara ya mwisho kwa Ureno kufunga magoli mengi zaidi ilikuwa ushindi wa bao 8-0 dhidi ya Liechtenstein (1994 na 1999) pamoja na Kuwait mwaka 2003.
Mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or amecheza jumla ya michezo ya kimataifa 201 na kufunga magoli 123 ambayo hayajafikiwa na mchezaji yoyote katika historia ya soka, huku akiwa amefunga mabao matano kwenye michezo mitano ya aliyoshiriki Kombe la Dunia tangu mwaka 2022.