Fahamu

“Noti zetu za Tanzania zimetengenezwa namna ambayo haziwezi kuhifadhi na kueneza virusi vya Corona – BOT

"Noti zetu za Tanzania zimetengenezwa namna ambayo haziwezi kuhifadhi na kueneza virusi vya Corona - BOT

Kauli ya Benki kuu ya Tanzania BoT kuhusu fedha zetu za noti kueneza virusi vya Corona “Noti zetu zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti, hata hivyo kwa kuwa noti hizo zinapita katika mikono mingi, tunawashauri Wananchi kuzingatia miongozo ya kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni au sanitizer”-Benki Kuu ya Tanzania (BOT)

“Katika kipindi hiki ambacho tuna janga la corona, tunawashauri Wananchi kufanya miamala kwa kutumia njia mbadala za malipo kama simu za mkononi, intaneti na kadi bila kulazimika kufika kwenye kaunta za benki au ATM kuchukua noti”


“Corona ni tishio Duniani kote na tayari Tanzania tuna wagonjwa watatu, tunawasihi Wananchi katika kipindi hiki ambacho Taifa linapambana na corona kuzipuuza taarifa zinazozagaa mitandaoni ambazo hazina vyanzo vya uhakika, zinazozihusisha noti zetu na usambazaji wa corona”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents