Habari

Nsekela atembelea na kukabidhi zawadi wodi ya wazazi hospitali ya Taifa Muhimbili

Katika kuadhimisha Wiki ya Mtoto wa Afrika, Benki ya CRDB imefanya tukio maalum la kugawa zawadi na kufungua akaunti kwa watoto 71 waliolazwa katika wodi namba 40, 41 na 42 za Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Akizungumza katika tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na taasisi za afya kama Muhimbili katika kuhakikisha jamii inapata huduma bora si tu za kifedha, balipia kijamii. “Watoto ni hazina ya Taifa. Tunatambua Wajibu wetu wa kijamiïi katika kuhakikisha wanapata huduma bora za afya na elimu ya kifedha mapema. Tutaendeleza ushirikiano wetu na Muhimbili ili kuhakikisha kuwa tunafanikisha lengo la kila Mtanzania kupata huduma bora,”‘ amesema Nsekela.

Aidha, Nsekela ametumia nafasi hiyo kuipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa utoaji wa huduma bora za afya nchini ambapo pia amempongeza aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Mohammed Janabi kwa kazi nzuri na kwabkuchaguliwa kwake kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika. Nsekela pia alitoa pongezi kwa Dkt Delilah Kimambo kwa kuteuliwa kwake kuwa MkurugenziMtendaji mpya wa Muhimbili, akiahidi kuendeleza ushirikiano baina ya taaisisi hizo.

Kwa upande wake, Profesa Mohamed Janabi ameishukuru Benki ya CRDB kwa mchango wao mkubwa kwa jamii ikiwamo sekta ya afya. “Nawapongeza Benki ya CRDB kwa moyo wao wa kujitolea kusaidia watoto na jamii kwa ujumla. Ushirikiano kama huu unadhihirisha dhamira ya kweli ya taasisi binafsi kushirikiana na umma katika kuinua huduma za afya nchini,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents