Nyama choma sasa yatambuliwa kama neno la Kiingereza

Neno nyama choma ambalo hutumika sana katika milo inayopendwa na wananchi wa mataifa ya Afrika Mashariki sasa limejumuishwa katika kamusi ya kiingereza.

Hii ni baada ya wachapishaji wa Oxford University Press (OUP) kujumuisha neno hilo na maneno mengine 47 ya Afrika Mashariki katika toleo lake la 10 la Kamusi ya Kiingereza.

Maneno mengine yaliyojumuishwa katika toleo jipya la kamusi hiyo ni pamoja na isikuti,ambalo ni la jamii ya Kiluhya Magharibi mwa Kenya ,kayamba, Maasai, majimbo na zeze.

Oxford University Press (OUP) pia amefanyia maboresho toleo lake la nne la Kamusi ya Kiswahili Sanifu (kamusi ya Kiswahili) ili kujumuisha maneno zaidi ya 1,000 na kuwa na kurasa mpya 48.

Mchapishaji alisema kuwa maneno ya nyongeza sasa yanakubaliwa kimataifa kutumiwa katika mwingiliano rasmi ikiwa ni pamoja na katika mazingira ya shule.

Toleo la hivi karibuni la OALD linakuja miaka 73 baada ya ile ya kwanza kuchapishwa na OUP, wakati toleo la nne la Kamusi ya Kiswahili ambalo limetolewa miaka 40 baada ya kuchapishwa mara ya kwanza.

Related Articles

Back to top button