Nyota Ndogo akanusha kuwa na ujauzito wa mtoto wa tatu

Muimbaji wa nchini Kenya Nyota Ndogo amekanusha ripoti zilizoenea kuwa ni mjamzito.

Mama huyo wa watoto wawili na mwenye miaka 31 aligeuka kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na madai kuwa anategemea kupata mtoto wa tatu.

Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Mwanaisha Abdallah alikiambia kituo kimoja cha radio mjini Mombasa kuwa, “Nimenepa tu na nipo kwenye hatua katika maisha yangu ambapo nimerelax. Ni mapema mno kwangu kuwa na mtoto wa tatu. Mtoto wangu wa pili ndio ana miaka miwili sasa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents