HabariMichezo

Nyota wa Arsenal, Pablo Mari jana alikimbizwa hospitalini baada ya kuchomwa kisu

Mtu mmoja ameuawa na wengine wapatao watano wamejeruhiwa – baadhi yao vibaya – katika shambulio la udungaji wa visu katika soko la bidhaa mbali mbali- supermarket, karibu na mji wa Italia wa Milan, polisi wamesema.

Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30, mfanyakazi wa duka alifariki baada ya mwanaume kuanza kuwashambulia watu katika Assago.

Miongoni mwa majeruhi alikuwa ni Pablo Mari, mchezaji soka anayecheza kwa mkopo kutoka Arsenal.

Mshukiwa mwenye umri wa miaka 46 – amekamatwa. Polisi wamesema halikuwa halikuwa shambulizi lenye nia ya ugaidi.

Taarifa zinasema mshambuliaji alikuwa na matatizo ya afya ya akili na alinyakuwa silaha hiyo kutoka kwenye duka hilo .

Mwanaume huyo alianza kuwadunga kisu watu kiholela majira ya saa kumi na mbili unusu jioni kwa saa za Italia (16:30 GMT) katika duka la Carrefour lililopo kwenye kituo cha mauazo ya bidhaa mbali mbali.

Kelele ziliripotiwa kusikika ndani ya kituo hicho, huku wanunuzi waliokuwa na hofu wakitoroka kutokana na wasi wasi

Mshambuliaji ameripotiwa kuwa alikuwa amekamatwa na wateja kadhaa na kumkabidhi kwa polisi ambao waliwasili katika eneo la tukio.

Image caption: Pablo Mari alijiunga na Monza kwa mkataba wa mkopo mwezi Agosti

Mari, mwenye umri wa miaka 29-mlinzi Mhispania, alipata majeraha ya kisu mgongoni – lakini majereha yake hayatishii maisha. Wakala wake, Arturo Canales, alisema kwamba alikuwa mwenye ufahamu na hakuna kiungo chake muhimu kilichoathiriwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents