Makala

Nyumba ya Bibi Kidude yauzwa, Wananchi wapingana na uamuzi huo(Video)

Mtaa wa Raha Leo ulipata umaarufu mkubwa Zanzibar kutokana mkongwe wa muziki wa taarab Fatma Binti Baraka maarifu kama Bi. Kidude ambaye alifariki dunia mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 103.

“Yalaiti napenda pasi kifani tofauti sikutilii moyoni sikuachi leo na kesho peponi…” ni sehemu ya mashairi yaliyopo kwenye wimbo uitwao Yalaiti, wa ‘Bi Kidude ambao ulimpatia umaarufu mkubwa ndani ya nchi na Kimatafa.

Wiki hii Bongo5 ilitembelea Zanzibar na kutembelea eneo hilo na kukuta mambo yamebadilika. Majirani wa miaka hii ambao wanaishi maeneo hayo wamedai hawajui kama eneo hilo kuna mkongwe huyo alikuwa akiishi.

Baada ya kufika kwenye nyumba ya Bi Kidude, tuliikuta familia mpya ambayo imepanga wakidai nyumba hiyo ya marehemu iliunzwa na ndugu kwa mmiliki mwingine na yeye akabomoa nyumba ya Bi Kidude na kujenga nyumba mpya ambayo wamepanga.

Wapangaji hao wamedai wamekuwa akipokea watu wangi wakidai hapo ni nyumbani kwa mkongwe huyo na wao wamekuwa wakiwaelewesha.

Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamekiri utambulisho wa mtaa huo kwamba aliishii mkongwe huyo unaendelea kupotea huku wakiitaka serikali ya Zanzibar kufanya kitu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents