Obama kutoa dola milioni 2 kusaidia vijana

Aliyekua rais wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle Obama, wametangaza kupitia taasisi yao ya Obama Foundation kwamba, watatoa kiasi cha Dola za kimarekani milioni mbili kwa ajili ya kuwasaidia vijana katika enero la south side Chicago.

Fedha hizo zitaelekezwa kusaida upatikanaji wa ajira kwa vijana hao kwa kuendesha warsha mbalimbali za kuwasaidia mbinu za upataji kazi. Obama aliyazungumza hayo katika uzinduzi wa ‘Obama Presidential Library’, jengo ambalo serikali yake inamjengea, na ambapo makao makuu yake kikazi yatakua hapo Chicago. Ofisi zake za Obama Foundation pia zitapatikana hapo. Ujenzi wa jengo hilo unakadiriwa kuchukua miaka minne.

Obama amesema wanatarajia kuanza kazi za kuihudumia jamii kuanzia sasa na hawatasubiri miaka minne ya ujenzi wa ofisi za taasisi yake kama ilivyokua kwa marais waliopita.

Hatua ya Obama kutoa fedha hizo inatokana na Rais wa sasa, Donald Trump kufuta program aliyoianzisha Michelle Obama ya kuwasaidia watoto wa kike kupata fursa za elimu duniani kote, iliyojulikana kama ‘Let Girls Learn’.

Related Articles

Back to top button