BurudaniHabari

Obby Alpha msanii tishio kwenye muziki wa Injili Tanzania

Moja kati ya wasanii wanaofanya vizuri kwenye Tasnia ya muziki wa Injili Tanzania kwa mwaka huu ni Obby Alpha na wimbo wake wa Washangaze.

Yes! Licha ya kuwa na nyimbo nyingi zilizomtambulisha, lakini wimbo wake wa washangaze umepokelewa kwa ukubwa zaidi na wadau wa muziki huo.

Akiongea na Bongo5, @obbyalpha amesema huu ni mwanzo mzuri kwake na kuahidi kufanya kazi nzuri zaidi mwakani.

“Unajua Muziki wetu ni Huduma kwa wasikilizaji wetu, Lakini kama Msanii ukiona kazi zako zinapendwa na watu wengi lazima utafurahi kwani hayo ndio mafanikio na naamini mwakani nitafanya vizuri zaidi ya hapa”, amesema Obby Alpha.

Kuhusu kuachia kazi nyingine ya kufunga mwaka 2022, @obbyalpha amesema kwasasa ana video 10 ambazo zipo tayari hivyo ni suala la muda tuu.

“Naishukuru sana Menejimenti yangu, Kwani tunafanya kazi kiuweledi. Hii inanifanya nifanye kazi katika mazingira rafiki zaidi, Kuwa na video 10 tena zimeongozwa na Ma-Directors wakubwa hapa Tanzania sio kazi rahisi hususani kwasisi waimbaji wa Injili”, Amesema Obby Alpha.

Kwasasa Obby Alpha (@obbyalpha) anafanya vizuri sana na video ya wimbo wake mpya wa Washangaze, Bofya link hapa chini kuitazama video hiyo.
Unaweza pia kutazama kazi zake nyingine kwenye Digital Platforms mbalimbali anatumia jina la @obbyalpha.

#bongo5updates #gospel

Related Articles

Back to top button