AfyaHabari

Ocean Road yapokea msaada wa barakoa 2000 za upasuaji (+Video)

Hospitali ya Ocean Road imepokea msaada wa barakoa za upasuaji 2000 kutoka kampuni ya utengenezaji na usambazaji ya vifaa tiba ya Aleka Holdings.

Akizungumza wakati wa upokeaji wa barakoa hizo Muuguzi Kiongozi Hospitali ya Ocean Road, Chausiku Chapuchapu ameishukuru kampuni hiyo kwa kuguswa kwao  ”Tumepokea msaada huu wa barakoa za upasuaji kwa moyo wa furaha na tunawashukuru sana wenzetu wa Aleka Holdings. Serikali yetu inafanya kazi kubwa kwenye huduma za afya lakini kwa sekta binafsi kuja kutuunga mkono ni kitu cha kushukuru sana.”

Naye mwakilishi wa Aleka Holdings amesema ”Tunaunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata huduma kwa gharama nafuu. Tunafanya kazi ambayo inagusa moja kwa moja maisha ya watu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents