Nahodha wa Uganda Cranes, @emmanuelokwi amekamilisha usajili wake wa kuwatumikia Mabingwa mara nne wa Ligi Kuu nchini Iraq Klabu ya Erbil SC.
Okwi amejiunga na timu hiyo ya Erbil SC akitokea Klabu ya Zawraa SC.
Anakuwa Mganda wa nne kuwahi kuitumikia Klabu hiyo ya Erbil SC baada ya Sula Matovu, Ivan Bukenya na Allan Kateregga.
Erbil inakuwa ni timu ya nane kwa Emanuel Okwi nje ya Uganda zikiwemo Simba SC, Young African, Etoile Du Sahel (Tunisia), Sonderjyske (Denmark), Al Ittihad (Misri).
Imeandikwa na @fumo255