Afya

Ommy Dimpoz, Lipumba na Prophet Trizah wachanjwa chanjo ya Corona (+ Video)

Baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kutangaza kuwa Chanjo ya Corona ipo anayetaka akachanjwe ili iweze kukusaidia kwenye harakati zako mwitiko unekuwa mkubwa kwani baadhi ya watu wameanza kuchanjwa.

Siku ya kwanza kabisa baada ya kauli hiyo Mwenyekiti wa CUF IBRAHIM LIPUMBA alienda kuchanjwa na huyu ni staa wa Bongo Fleva @ommydimpoz akichukua chanjo.

Lakini pia  kiongozi wa Kanisa la Rehema The Faithful Church anaitwa Prophetess/Nabii @prophetess_trizah ameshachanjwa kwa ajili ya kujilinda na gonjwa hatari la Corona.

Watanzania mnashauriwa kwenda kuchanjwa kwa ajili ya kujikinga na Corona lakini pia kwa wale wanaosafiri nje ya Nchi kuna baadhi ya Mataifa ambaye yameweka shwria kali kwamba bila kuwa na cheti cha chanjo huwezi kuingia kwenye taifa hilo.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents