FahamuHabari

Operesheni ya siku mbili yaua Magaidi 40

Jeshi la Mali limesema limewauwa takribani Magaidi 40 na kuharibu moja ya Ngome zao katika Operesheni mbili zilizofanyika nchini humo.

Operesheni ya Alhamis katika mji huo iliharibu ngome moja na kuwauwa takribani magaidi 30 huku risasi, silaha na pikipiki 24 zikikamatwa, wakati operesheni iliyofanyika Ijumaa ilifanikisha kuuwawa kwa wanamgambo 10 pamoja na kukamatwa bidhaa kadhaa ikiwemo magari na pikipiki.

Mali ambayo inakabiliana na migogoro ya kisiasa, imekuwa ikiandamwa na makundi ya Kigaidi ya Al-Qaeda na lile linalojiita dola la Kiislamu tangu mwaka 2012.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents