Burudani
P Diddy ashtakiwa kwa Kumbaka mtoto wa miaka 10

Rapa wa Marekani Sean Combs maarufu P Diddy anakabiliwa na tuhuma mpya za kumlazimisha mtoto wa miaka 10 kufanya kitendo cha kingono ili kupata nafasi ya kuwa Staa.
Tuhuma hizi zimeibuliwa kwenye kesi mpya iliyowasilishwa Jumatatu na mlalamikaji anayetajwa kama John Doe akimshtaki rapa huyo kwa kumpa dawa za kulevya na kumdhalilisha kingono mvulana wa miaka 10 katika chumba cha Hoteli mjini New York mwaka 2005.
Wimbi la kesi nyingi kumhudu Diddy ambaye anashikiliwa na Polisi limezidi kuongezeka huku washtaki wengi wakidai walinyanyaswa kingono na mwanamuziki huyo licha ya Mwanasheria wake kukanusha madai hayo na kumshutumu wakili wa walalamikaji.