Michezo

Pablo Franco afungiwa na faini juu

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Januari 27, 2022 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi yafuatayo.

Pablo Franco apewa mbinu kombe la Shirikisho | East Africa Television

Kocha wa timu ya Simba, Pablo Franco amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya shilingi 500,000 (laki tano) kwa kosa la kupiga teke chombo maalum cha kuhifadhia barafu/ vinywaji vya baridi wakati mchezo tajwa hapo juu ukiendelea.

Hii ni mara ya pili kwa kocha Pablo kufanya tukio la namna hii ambapo mara ya kwanza alipewa onyo baada ya kupiga teke kiti katika mchezo wa timu yake dhidi ya timu ya KMC uliofanyika kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Adhabu hii ni uzingativu wa Kanuni ya 45(2.2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Lakini pia Kocha Pablo Franco ametozwa faini ya sh 1000,000 (milioni moja)  kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na Wanahabari mara baada ya mchezo huo kumalizika.

Adhabu hii imetolewa na kwa mujibu wa kanuni ya 45(2.13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Mechi namba 69; Kagera Sugar 1-0 Simba SC Kocha Pablo Franco ametozwa faini ya sh 1000,000 (milioni moja) kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na wanahabari mara baada ya mchezo tajwa hapo juu kumalizika.

Mechi namba 96; Mbeya City 1 – 0 Simba SC, Kocha Pablo Franco ametozwa faini ya sh 1000,000 (milioni moja) kwa kosa la kufanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo kumalizika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents