HabariMichezo

Panga la wachezaji Simba SC, wazee wa benchi wakalia kuti kavu

Kumekuwa na malalamiko mara kwa mara kutoka kwa baadhi ya mashabiki na wadau wa soka nchini kuhusu Wachezaji wa Simba kudaiwa kuwa hawajitumi uwanjani ukilinganisha na wale wa Yanga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amethibitisha kuwa wapo wachezaji ambao watapoteza nafasi zao.

Try Again amesema hayo kupitia Azam tv kuwa wachezaji ambao hawataonesha walichonacho basi ule msemo maarufu wa ‘Thank You’ utawahusu.

”Tutafanya marekebisho kwenye timu yetu, kuna wachezaji ambao watapoteza nafasi zao, Simba haiwezi kukaa na kusubiri inahitaji mafanikio, kwa wale ambao hawataonesha walichonacho Thank You itawahusu. Hatuna sababu ya kuwa na wachezaji ambao wanalipwa vizuri halafu wanakaa Benchi.”

Huwenda dirisha dogo lijalo la usajili tukashuhudia baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa wakaachwa Msimbazi.

Je, Simba wafanye nini kurudi kwenye ubora wao wa ‘Pira Biriani’.?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents