Habari

Panya aiba mkufu wa almasi mbele ya ulinzi mkali (+Video)

Kutana na Panya mwizi aliyeweza kuvuka vikwazo vyote vya ulinzi vilivyowekwa kwenye duka hili la vitu vya urembo na vyenye thamani kubwa mpaka kufanikiwa kuiba Mkufu wa Almasi.

Tukio hilo limetokea Delhi, India kwenye duka la vitu vya urembo na panya huyo kuondoka na mkufu huo licha ya kunaswa na CCTV Kamera lakini aliweza kumudu kutekeleza wizi huo na kutoroka na cheni pasipojulikana.

VIDEO BOFYA HAPA

Baadhi ya wafanyakazi dukani hapo walituhumiwa kwa tukio hilo la wizi kabla ya kupitia mifumo ya ulinzi pamoja na video za CCTV ndipo walipogundua mwizi wao alikuwa ‘PANYA’.

Kumekuwa na stori tofauti miongoni mwa waliona video hiyo, wapo wanaoamini katumwa na wengine kuamini imani za kishirikina.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents