Fahamu

Panya wa Tanzania mwenye uwezo wa kutegua mabomu kimataifa astaafu Cambodia (+ Video)

Magawa panya aliyejishindia tuzo kwa ushujaa wake anastaafu katika kazi yake ya kufichua mabomu yaliotegwa ardhini. Katika kazi ya miaka mitano aliofanya , panya huyo alifanikiwa kugundua mabomu 71 yaliotegwa ardhini pamoja na vilipuzi kadhaa nchini Cambodia.

Lakini wasimamizi wake wanasema kwamba panya huyo mwenye umri wa miaka saba ameanza kupungiza kasi yake akielekea kuwa mzee na anahitaji kuheshimu mahitaji yake.

Imedaiwa kwamba kuna takriban mabomu sita ya ardhini katika taifa hilo la kusini mashariki mwa bara Asia.

 

Magawa alifunzwa na shirika la uhisani la Apopo nchini Ubelgiji lenye makao yake nchini Tanzania, ambalo limekuwa likiwalea wanyama hao wanojulikana kama HeroRATS{Panya shujaa} kubaini mabomu ya ardhini tangu 1990.

Wanyama hao hupewa vyeti baada ya kufunzwa kwa mwaka mmoja.

Wiki iliopita, Apopo lisema kundi jipya la panya wachanga limechunguzwa na kituo cha kutegua mabomu nchini Cambodia na wamefaulu kwa kiwango cha juu.

Malen na Magawa

Magawa, kundi hilo lilisema , atasalia nchini humo kwa wiki chache zaidi ili kuwakuza panya hao wachanga kwa lengo la kuwasaidia kuzoea mazingira hayo.

“Utendakazi wa Magawa haujashindwa na najivunia kufanya kazi naye”, alisema Malen.

”Ni mdogo lakini amesaidia katika kuokoa maisha mengi akitusaidia kuwarudishia watu wetu ardhi ilio salama kwa haraka zaidi”.

Je mabomu yakiotengwa ardhini yako wapi?

Septemba iliopita Magawa alituzwa medali ya PDSA – inayoelezewa kuwa ya jasiri wa kuokoa maisha.

Alikuwa panya wa kwanza kutuzwa medali hiyo katika historia ya miaka 77 ya shirika hilo la uhisani.

Ana uzani wa kilo 1.2 na urefu wa inchi 28.

Huku vipimo hivyo vikiwa ni vile vya panya mkubwa ikilinganishwa na panya wengine, Magawa ni mdogo na mwepesi kutosha kuweza kutegua mabomu anapopita juu yake.

Panya hao hufunzwa kufichua kemikali fulani ndani ya vilipuzi, ikimaanisha kwamba hupuuza vyuma na wanaweza kugundua mabomu kwa haraka sana.

Wanapopata kilipuzi , hukuna juu juu na kumtahadharisha msimamizi wake .

Magawa ana uwezo wa kutafuta mabomu katika uwanja ulio na ukubwa kama ule wa mchezo wa tenisi kwa dakika 20 pekee – kitu ambacho Apopo inasema itamchukua mtu mwenye kifaa cha kubaini vyuma siku moja hadi nne.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CPuq4W5BwCI/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents