FahamuHabari

Papa Francis ataka mateka wa Israel waliotekwa na Hamas waachie mara moja

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, katika matamshi yake makali tangu kuanza kwa mzozo kati ya Palestina na Israel, ametoa wito wa kuachiliwa kwa Mateka wote waliochukuliwa na wanamgambo wa Hamas na kusema Israel ina haki ya kujilinda.

Mtandao wa @DW_Kiswahili umeripoti kuwa akiongea mwishoni mwa hadhara yake ya kila wiki kwa maelfu ya Watu katika uwanja wa St. Peter, Papa Francis ameelezea pia wasiwasi wake juu ya kuzingirwa kwa Israel na Gaza.

“Ninaendelea kufuatilia, kwa uchungu na wasiwasi kile kinachotokea Israel na Palestina, Watu wengi sana wameuawa na wengine kujeruhiwa, naziombea Familia zilizoshuhudia siku ya sikukuu ikigeuka kuwa siku ya maombolezo na ninaomba kwamba Mateka waachiliwe mara moja”

“Ni haki ya wale wanaoshambuliwa kujilinda, lakini nina wasiwasi mkubwa na mzingiro mzima wa Wapalestina wanaoishi Gaza, ambako pia kumekuwa na wahasiriwa wengi wasio na hatia”

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya ndege usiku kucha katika viunga vya ukanda wa Gaza, huku vita vyake dhidi ya kundi la Hamas vikiingia siku ya tano leo Jumatano na zaidi ya Watu 2,200 wameuawa katika vita hivyo kwa pande zote huku vifo vikihisiwa kuongezeka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents