Habari

Papa Francis: Bado nipo hai

Papa Francis ametania kuwa “bado yuko hai” alipokuwa akiondoka hospitalini mjini Roma baada ya kukaa kwa siku tatu.

Alilazwa katika Hospitali ya Gemelli katikati ya wiki akiwa na matatizo ya kupumua.

Vatican ilitoa taarifa kuwa atatoka leo Jumamosi, kulingana na matokeo ya vipimo.

“Sikuwa na hofu, bado niko hai,” papa huyo mwenye umri wa miaka 86 aliwaambia waandishi wa habari na waombezi wa heri nje ya hospitali kabla ya kuruhusiwa kuondoka hospitali.

Alionekana akitabasamu na kupunga mkono kutoka kwenye gari, kabla ya kutoka nje kuzungumza na umati. Kisha akaelekea Vatican.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents