
Klabu ya Ligi Kuu ya NBC ya Singida Fountain Gate FC imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Pascal Serge Wawa.
Uamuzi huo umefanywa na Shirikkisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya Wawa kushinda kesi ya madai dhidi ya Klabu hiyo.
Mchezaji huyo raia wa Ivory Coast alifungua kesi FIFA alidai malipo ya ada ya usajili (sign on fee) na malimbikizo ya mishahara.
Klabu hiyo ilitakiwa iwe imelimlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo. Wakati FIFA imeifungia Klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.