Michezo

Petro Atletico yamtema Carlinhos

Klabu ya Petro Atletico imeachana na Kiungo wake, kiungo wa zamani wa Yanga SC, Carlos Stenio Fernandes Guimaraes do Carmo maarufu kama Carlinhos huku sababu kubwa ikiwa ni vitu vya nje ya Uwanja na wala sio kutokana na kiwango chake.

Duru mbalimbali nchini Angola zinaeleza kuwa Carlinhos ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ila mambo ya nje ya uwanja ndiyo yanayofanya asiwe nyota mkubwa Afrika.

Klabu ya Cape Town City ya nchini Afrika Kusini imefikia makubaliano ya kumsajili Carlinhos kutokea Petro De Atletico ya Angola.

Carlinhos (29) raia wa Angola anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja wenye chaguo kuongezeja na tayari amefanyiwa vipimo vya afya.

Carlinhos Carmo aliondoka Young African SC kwa makubaliano ya pande mbili kwa sababu za nje ya Uwanja pia

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B,.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents