Burudani

Picha: Drake aongeza namba ya warembo, aibuka na mzigo mzito

Baada ya Drake kudaiwa kuwa na mahusiano na mrembo Malaika Terry, wiki hii rapper huyo ameonekana kuibuka na chombo kipya tena ni moto wakuotea mbali.

Drake ameonekana akitoka kwenye mgahawa wa Sotto Sotto uliopo mjini Toronto, Canada akiwa na mrembo ambaye anafahamika zaidi kwenye mtandao wa Instagram kwa jina la Zmeena.

Japo haijafahamika kama wawili hao ni wapenzi kwa sasa, lakini picha ambazo wamepigwa zimeonekana kusambaa zaidi kutokana na mrembo huyo alivyoumbika na umbo lake la kuwatoa vidume udenda.

Baadhi ya mashabiki wanamini Drake kuwa na mahusiano na mwanadada huyo kutokana na kujigamba kwake kwenye ngoma ya Nicki Minaj ‘Only’ ambayo alimshirikisha Drake, Lil Wayne na Chris Brown.

“I like my girl BBW, yeah type to wanna suck you dry and then eat some lunch with you,” amerap Drake kwenye ngoma hiyo.

Related Articles

Back to top button