Burudani

Picha: Huu ndio mjengo aliouacha rapper XXXTentacion, gharama yake ni kufuru

Licha ya rapper XXXTentacion kudaiwa kuwa na kesi lukuki enzi za uhai wake, lakini ameweza kujenga mjengo wa ndoto zake za muda mrefu.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, XXXTentacion alitumia kiasi cha dola milioni 1.4 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni tatu za Kitanzania kujenga jumba hilo la kifahari ambalo lipo maeneo ya Parkland mjini Florida na ni mwendo wa dakika 15 kutoka eneo ambalo ameuawa kwa kupigwa risasi.

Mjengo huo unatajwa kuwa na vyumba vinne vya kulala, mabafu 5 ya kuoga, bwawa la kuogelea na eneo kubwa la kiwanja ambalo lipo wazi.

Majirani wa msanii huyo wameumbia mtandao huo kuwa, XXXTentacion alihamia hivi karibuni kwenye nyumba yake hiyo na alikuwa ni mkimya lakini ni rafiki wa kila mtu.

Rapper huyo amefariki Jumatatu hii kwa kupigwa risasi wakati akitoka kwenye duka la pikipiki mjini Florida.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents